Tuesday, June 30, 2009

A

Amri bila tafakuri ni ubaradhuli.
Asiyetafuta hapati.
Asiyeomba hapewi.
Asiyetatua tatizo yeye mwenyewe tatizo.
Akili hasara.
Akili balaa.

B

Bia maji, ulevi mkojo.
Bure ghali.
Benki si jengo bali huduma.
Buzi mwananchi, mchunaji kiongozi.

C

China soko, tafuta biashara.
Chama biashara, hula hakiliwi.
Choo kingelisema nani angelikuwa na siri?
Chumba kidogo kwa nyumba, na kaburi dogo kwa chumba.
Chakula kwa sahani, mla mbili mlafi.
Chuma ulete hadithi, mdokozi ni wewe.
Chema chajitembeza, kibovu chajiuza.

D

Dua la kuku humpata mwewe!
Dhuluma hujilipa yenyewe
Dobi hajifui, hukoga.
Dodo halifanani na boribo kwa ladha.
Dunia kiti kibovu.

E

Eda sio kwa mzee hata kwa kijana pia.
Enzi zile sio hizi.
Ezeka paa imara, pepo dhaifu zisiezue.
Endelevu si mradi bali watu.

F

Faida roho ya biashara.
Furaha usoni, moyoni roho mbaya.
Fusso sio basi na basi sio fusso.
Fumbo mfumbie kiongozi, mwananchi ataling'amua.

G

Giza la nje, huleta nuru ya ndani.
Gari kipando sio shoorumu.
Gari kipando sio disko.
Garimoshi umeme na gesi sio mkaa.