Tuesday, June 30, 2009

A

Amri bila tafakuri ni ubaradhuli.
Asiyetafuta hapati.
Asiyeomba hapewi.
Asiyetatua tatizo yeye mwenyewe tatizo.
Akili hasara.
Akili balaa.

B

Bia maji, ulevi mkojo.
Bure ghali.
Benki si jengo bali huduma.
Buzi mwananchi, mchunaji kiongozi.

C

China soko, tafuta biashara.
Chama biashara, hula hakiliwi.
Choo kingelisema nani angelikuwa na siri?
Chumba kidogo kwa nyumba, na kaburi dogo kwa chumba.
Chakula kwa sahani, mla mbili mlafi.
Chuma ulete hadithi, mdokozi ni wewe.
Chema chajitembeza, kibovu chajiuza.

D

Dua la kuku humpata mwewe!
Dhuluma hujilipa yenyewe
Dobi hajifui, hukoga.
Dodo halifanani na boribo kwa ladha.
Dunia kiti kibovu.

E

Eda sio kwa mzee hata kwa kijana pia.
Enzi zile sio hizi.
Ezeka paa imara, pepo dhaifu zisiezue.
Endelevu si mradi bali watu.

F

Faida roho ya biashara.
Furaha usoni, moyoni roho mbaya.
Fusso sio basi na basi sio fusso.
Fumbo mfumbie kiongozi, mwananchi ataling'amua.

G

Giza la nje, huleta nuru ya ndani.
Gari kipando sio shoorumu.
Gari kipando sio disko.
Garimoshi umeme na gesi sio mkaa.

H

Hakika yako sio hakika ya mwenzio.
Hoja si nguvu na nguvu si hoja.
Hadimu fukara kwa tajiri.
Hofu mama wa makosa.
Hiari bila tijara dhuluma.

I

India letu soko, katafute biashara.
Ingiza utoe, ukitoa tu hakijai.

J

Jamii isiyoteta, jamii iliyokufa.
Jinsia uchumi, waume na wake hali.
Jina utu sio ukubwa au utajiri.
Juhudi sio mafanikio [haki isipokuwepo].

K

Kiswahili mtaji, kutajirika tuwekeze.
Kiongozi ni mtwana, hawezi kuwa bwana!

L

Lugha ya kuazima haimjengi Mwafrika.
Lugha kipimo cha akili. [Ikisemwa na kutumika katika shughuli kwa asilimia 5 ya watu nchini na nchi nayo ina akili asilimia 5 tu. Ikisemwa na kutumika katika shughuli kwa asilimia 95 ya watu na nchi nayo inakuwa ina akili asilimia 95.]

M

Mali na wana mtihani.
Mmoja tajiri, wengi kampuni.
Mvaa mbili havai moja.
Maiti si bora kuliko mgonjwa.
Mfu kamzikeni, mgonjwa wangu.
Mpende akiwa hai sio akiwa maiti.
Mtanzania haishi atakavyo bali awezavyo!

N

Njia iliyonyooka, sio njia sahihi.
Nyumba si anasa, bali hitaji la msingi.
Nauli nusu, mwanafunzi mtu kamili.

O

Ongezeko mali, watu ufukara.
Onja isiyo na mwisho sio onja ni ufujaji.
Ona usiseme na halitakupata jambo.

P

Papa baharini, nchi kavu nguru.
Pua hunusa, macho huona na mdomo humeza.
Pipa kujaa nusu, bora kuliko pungufu.
Ponda mali umasikini waja.
Pendo jipende mwenyewe.

R

Rai ushauri, ari jeuri!
Rais kofia, baraza lake mwili.
Raila asipokula, kibaki hatabakisha.

S

Subira ikipita kiasi shubiri.
Sifuri ilizaa dunia.
Saa lengo, ahadi shabaha.

T

Tiba huanzia na usafi wa mwili na mazingira.
Tatizo, fursa.

U

Ukimwi zao, zinaa mbegu.
Utu bora kuliko mali.
Ubinadamu vitendo sio maneno.

V

Viatu sio watu, na watu sio viatu.

W

Wa kulia wa kulia, wa kushoto

wa kushoto.
Walimu walezi, walee wawalee

wanao.

Y

Yako, yako, yangu, yangu,kishaye wako sio wangu!

Z

Zito sio jepesi, tofauti zao kasi.